Breaking News

MWEKEZAJI BAKARI NYOROBI AUTAKA UDIWANI KATA YA PANZUO MKURANGA

Mwekezaji Bakari Nyorobi akionesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya udiwani Kata ya Panzuo kupitia CCM.

........................................

Na Dotto Mwaibale

MWEKEZAJI Bakari Nyorobi amechukua fomu ya kuomba kugombea Udiwani Kata ya Panzuo iliyopo Tarafa ya Mkamba Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo atapambana na diwani aliyemaliza muda wake, Dude Hamisi Dude anayetetea nafasi   hiyo.

Wagombea wengine ambao wametajwa kuwania nafasi hiyo ni Getruda Mpelembe,  Iliasa Nyumba na wengine.

Mtia ni huyo Nyorobi anauzoefu wa masuala ya siasa kwani aliwahi kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Igunga Mkoa wa Tabora mwaka 2010 lakini katika mchakato wa kura za maoni hazikutosha na Lostam Azizi aliyekuwa akitetea nafasi hiyo aliibuka kidedea dhidi ya watia nia tisa kupitia CCM huku Nyorobi akiambulia kushika nafasi ya tatu.

Aidha, Nyorobi ni mfanyabiasha na mwekezaji  katika kata hiyo ambapo ana miliki heka zaidi 80 ambazo ndani yake kuna minazi na anatoa huduma nyingine za kijamii kama vile nyumba ya kulala wageni na biashara zingine ndogo ndogo.

Katika jimbo hilo hususan kata hiyo Serikali imefanya kazi kubwa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa jimbo hilo, Abdallah Ulega na diwani aliyemaliza muda wake, lakini kutokana na kuwepo kwa demokrasia watia nia hao wa nafasi hiyo wamejitokeza ili atakayefanikiwa kuwa diwani aendeleze  maendeleo kwenye maeneo  ambayo bado yana changamoto kwenye sekta mbalimbali.

Jimbo la Mkuranga hususan katika Kata hiyo linahitaji kupata viongozi wenye uwezo, maono na ubunifu ili liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya 2025/ 2030.


 Mwekezaji Bakari Nyorobi, Mtia nia nafasi ya udiwani Kata ya Panzuo Mkuranga Mkoa wa Pwani

No comments