Breaking News

BALOZI MAPURI: MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2025 YAZINGATIE SHERIA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Balozi Omar Ramadhan Mapuri  akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yalioanza leo Julai 21, 2025 Jijini Dar es Salaam.

...........................................

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetia msisitizo mkubwa na kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu yanafanyika kwa kuzingatia misingi ya sheria, maadili, na utulivu ili kuepusha malalamiko kutoka kwa washiriki wa uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Tume hiyo, Balozi Omar Ramadhan Mapuri wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yalioanza leo Jijini Dar es Salaam.

“ Ni sisitize kuwa utekelezaji wa majukumu ya uchaguzi unapaswa kuongozwa na katiba, sheria, kanuni na miongozo ya Tume na si vinginevyo,” alisema Balozi Mapuri.

Alisema Taifa linahitaji uchaguzi wenye amani, utulivu na unaoendeshwa kwa weledi wa hali ya juu na kuwa jambo hilo linawezekana kama kila mmoja atasoma kwa kina na kuelewa nyaraka zote muhimu za uchaguzi, na kuuliza maswali eneo ambalo hata kuwa hajalielewa vizuri.

Aidha, Balozi Mapuri amewataka wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha wanayaelewa mapema maeneo ambayo vitakuwepo vituo vya kupigia kura na kujua mahitaji mbalimbali.

Mafunzo hayo yameanza leo Julai 20, 2025 na kujumuisha washiriki 106 na yatafikia tamati kesho kutwa Julai 23, 2025 na ni mahususi kwa ajili ya kuwajengea uwezo waratibu wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo pamoja na wasimamizi na wasaidizi wa uchaguzi ili kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Mafunzo yakifunguliwa.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.

 Mafunzo yakiendelea.

No comments