Breaking News

BURIANI KATIBU WA CCM WILAYA YA MBOZI, JULIUS MBWIGA, AFARIKI SAA CHACHE KABLA YA KUSHIRIKI KIKAO MUHIMU

Bw. Julius Mbwiga, enzi za uhai wake

.......................................

Na Dotto Mwaibale

KATIBU wa Chama Cha Mapinzuzi (CCM) , Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe, Julius Mbwiga amefariki dunia leo Julai 6, 2025.

Kifo chake kimewasikitisha watu wengi waliokuwa wakimfahamu kutokana na uchapakazi wake uliotukuka.

Mbwiga amefariki dunia wakati akijiandaa kwenda kwenye kikao cha kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Mbozi mkoani humo ambacho kilipangwa kufanyika leo Julai 6, 2025.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa pole kwa ndugu jamaa, marafiki na viongozi wa chama hicho Mkoa wa Songwe.


 

No comments