MWENYEKITI WA UWT CHATANDA ATEMBELEA MABANDA YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI SABASABA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT),Mary Chatanda (katikati) akipunga mkono na wanawake wajasiriamali alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Julai 6, 2025 Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.
..............................................
Na Mwamdishi Wetu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Ndg. Mary Pius Chatanda ametembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam Leo Tarehe 6 Julai, 2025. Akiwa kwenye maonyesho hayo, Ndg. Chatanda alijifunza kuhusu majukumu na huduma zinazotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu; Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu; pamoja na taasisi mbalimbali zilizo chini ya ofisi hiyo.
Aidha, Ndg. Chatanda alitembelea mabanda ya wanawake wajasiriamali na kujionea ubunifu pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wanawake kutoka maeneo tofauti ya nchi. Akiwa katika mabanda hayo, alizungumza na baadhi ya wanawake waliopo kwenye biashara ndogondogo na za kati, akiwapongeza kwa juhudi zao na moyo wa kujituma katika kukuza Uchumi wa Mtu Mmoja Mmoja na Jamii kwa ujumla.
Akizungumza na Wanawake hao,Ndg. Chatanda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha Wanawake kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri. Na kusisitiza mikopo hiyo imekuwa kichocheo kikubwa kwa Wanawake kuanzisha na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi, na kuchangia Maendeleo ya Familia na Taifa kwa ujumla.
No comments