Breaking News

DC MPOGOLO: HAKUNA MWANAMKE ATAKAYEKOSA MKOPO UTAWALA WA RAIS SAMIA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, akizungumza, akizungumza Julai 25, 2025 jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kwa wanawake.

........................................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, ameendelea kusisitiza dhamira ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kila mwanamke mwenye haki na nia ya kweli ya kujiendeleza kiuchumi hapewi mgongo, bali anawezeshwa kwa njia ya mikopo na elimu ya kifedha.

Akizungumza Julai 25, 2025 jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa mikopo ya Halmashauri, Mpogolo amesema kuwa katika Wilaya ya Ilala, jumla ya vikundi 945 vya wanawake waliwasilisha maombi ya mikopo. Hata hivyo, baada ya kuhakikiwa, ni vikundi 449 pekee ndivyo vilivyokidhi vigezo vya kupatiwa mikopo. 

Vikundi vilivyokosa sifa hawakupuuzwa, bali wameanza kupewa elimu ya kina ili wajue walipokosea na waandaliwe upya kwa ajili ya fursa zinazofuata.

Katika hatua nyingine, wilaya hiyo imeamua kupeleka semina kata kwa kata, kuwafikia wanawake wote, kuwaelimisha kuhusu taratibu sahihi za kuomba mkopo, pamoja na kuwaunganisha na taasisi za kifedha zinazotoa mikopo rafiki.

Hii ni ishara ya dhahiri kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM, kwa kuweka mwanamke mbele kama nguzo ya maendeleo ya taifa. Kupitia usimamizi wa viongozi wake wa mikoa na wilaya, serikali inahakikisha hakuna mwanamke anayeachwa nyuma.

Ujasiri na uthubutu wa Mama Samia unaendelea kuleta mageuzi ya kweli kwa wanawake wa Kitanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, akisalimiana na wanawake katika mkutano huo.
Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Suleiman akizungumza kwenye mkutano huo
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ilala Bi. Francesca Makoy, akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Ukutano ukiendelea
Taswira ya mkutano huo.
Shamra shamra zikiendelea meza kuu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa Wanawake  Ilala Bi Rehema Sanga
 

No comments