MAPURI: KASIMAMIENI MAFUNZO MLIYOFUNDISHWA KWA KUZINGATIA, KATIBA, SHERIA NA KANUNI
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Balozi Omar Ramadhan Mapuri akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani yalioanza Julai 21, 2025 na kufikia tamati leo Julai 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.
....................................................
Na
Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
WARATIBU
wa uchaguzi, wasimamizi na maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani
wametakiwa kwenda kusimamia mafunzo waliyofundishwa kwa kuzingatia Katiba,
Sheria na Kanuni.
Hayo
yamesemwa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Balozi Omar
Ramadhan Mapuri wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa waratibu wa uchaguzi,
wasimamizi na maafisa kutoka mikoa hiyo yaliyofikia tamati leo Julai 23, 2025
Jijini Dar es Salaam.
“ Kasimamieni mafunzo mliyofundishwa kwa
kuzingatia Katiba, sheria na Kanuni na si vinginevyo,” alisema Mapuri.
Aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda
kuyatoa kwa wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata na watendaji wa
vituo vya kupiga kura kwa weledi wa hali ya juu.
Aidha,Mapuri aliwataka washiriki hao kwenda
kusimamia rasilimali na vifaa
watakavyopewa na Tume kwa ajili ya
utekelezaji wa kazi za uchaguzi na kuvihakiki vifaa hivyo mara tu watakapovipokea na kutoa taarifa
haraka kwa Tume iwapo kutakuwa na
upungufu.
Katika hatua nyingine Mapuri aliwataka washiriki
hao wa mafunzo hayo kwenda kusimamia
vyema matumizi ya fedha watakazotumiwa kwa ajili ya shughuli za
uchaguzi.
” Kura yako haki yako jitokeze kupiga kura”
No comments