Breaking News

MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZANA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA KAIBANJA


Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima, akikungumza na wananchi wa Kata ya Kaibanja alipokuwa akisikiliza kero zao mbalimbali alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi pamoja na Afisa Tarafa ya Katerero, Bwanku Bwanku Julai 9, 2025.

..............................................................

Na Mwandishi Wetu, Bukoba

Leo Jumatano Julai 09, 2025 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amefanya ziara kwenye Tarafa ya Katerero akiongozana na Afisa Tarafa wa Tarafa hiyo ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku kusikiliza na kutatua kero za wananchi Kata ya Kaibanja kwenye Kitongoji cha Kitundu, Kijiji cha Kiijongo.

Mkuu wa Wilaya Mhe. Erasto Sima alikutanisha pande zote zinazolalamikiana na kukaa nao chini kuwasikiliza na kuweka msisitizo wananchi kumaliza migongano yao na kuhimiza amani kwenye mazingira.

Pamoja nao, ziara hiyo ya kutatua kero za wananchi, Mhe. Sima aliongozana na Mtendaji wa Kata hiyo Ndugu Bruno Mathias na viongozi wa vijiji na vitongoji.

Afisa Tarafa wa Tarafa hiyo ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku akisisitiza jambo kwenye ziara hiyo.
Kero za wananchi zikipokelewa.
Kerozikitolewa
 

No comments