MUHIMBILI MLOGANZILA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VISION CARE TANZANIA KATIKA HUDUMA ZA MATIBU YA MACHO
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Upasuaji MNH-Mloganzila Dkt. Godlove Mfuko wakati alipokutana na kufanya majadiliano na taasisi hiyo kutoka nchini Korea Kusini.
Dkt. Mfuko ameongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu ambao umejikita katika kujengea uwezo wataalam, kusaidia vifaa tiba vya macho, na kugharamia huduma mkoba za macho kwa lengo la kusaidia wananchi husani katika mkoa wa Pwani.
Kwa upande wake mwanzilishi na Mwenyekiti wa taasisi Kim Donghae amesema taasisi hiyo itaendelea kushirikino na hospitali hiyo na inatarajia kuandaa kambi maalum ya macho Juni , 2026 ikiwa ni jitihada za kusogeza huduma za matibabu ya macho karibu na wananchi.
Hospitali ya Taifa Muhimbili–Mloganzila inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi ya macho ikiwemo upasuaji na kutengeneza miwani ambapo kliniki zake ni kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.
No comments