SUMA FYANDOMO ANG’ARA KURA ZA MAONI UBUNGE VITI MAALUMU MBEYA
Mhe. Suma Fyandomo
Mhe. Maryprisca Mahundi
............................................
Na Dotto Mwaibale
Waliokuwa Wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Suma
Fyandomo na Maryprisca Mahundi wametetea nafasi zao kwa kupata ushindi mnono
dhidi ya wagombea wenzao katika mchakato wa kura za maoni uliofanyika mkoani
humo.
Fyandomo ameibuka kidedea kwa kuongoza katika kinyang’anyiro
hicho na kumshinda Maryprisca Mahundi ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kura mbili.
Akitangaza majina ya washiriki na washindi wa mkutano huo wa
kura za maoni uliofanyika jana na kumalizika alfajiri ya leo Mkuu wa Mkoa
wa Kigoma Saimon Sirro ambaye alikuwa msimamizi wa mkutano huo alimtangaza Suma
Fyandomo kuwa ndiye aliongoza kwa kupata kura 1152, akifuatiwa na Maryprisca
Mahundi ambaye alipata kura 1150.
Wengine ni Ikupa Mwaifwani aliyepata kura 200, Tumaini
Mwakasege kura 45 na Sara Mwangasa aliyepata kura 189.
Wengine ni Hobokela Mwamkina aliyepata kura 72, Anna Mwangolombe aliyepata kura 7 na Upendo Kalasa aliyepata kura 18.
No comments