Breaking News

COLMAN MTIA NIA UBUNGE JIMBO LA KIVULE ILALA JIJINI DAR ES SALAAM


Anaelezea anavyozijua shida za wananchi


Mtia nia Ubunge Jimbo la Kivule Ilala Jijini Dar es Salaam, Colman Marwa, akionesha fomu baada ya kukabidhiwa.

...........................................

 Na Mwandishi Wetu

COLMAN Marwa si jina geni miongoni mwa wakazi wengi wa Jimbo jipya la Kivule lenye kata sita. Jimbo hilo ni miongoni mwa majimbo manane mapya yaliyozaliwa mwaka huu hapa nchini.

Si mgeni kwa sababu ameishi katika eneo hilo kwa muda mrefu na kuyafahamu vema maisha wanayoishi wakazi wake na changamoto wanazopitia. Anasema wakimchagua atawavusha

salama kwa sababu anaifahamu Kivule.

“Mimi nayajua vizuri matatizo ya wananchi wenzangu wa Kivule, barabara zetu kama mahandaki hasa kipindi cha mvua na baada ya mvua, maeneo ya kutolea huduma za afya, elimu na huduma nyingine za kijamii, rushwa imetawala,” anasema Marwa.

Marwa anayetia nia kugombea jimbo hilo kupitia Chama cha ACT Wazalendo, anasema akipitishwa kugombea na kushinda nafasi hiyo wapiga kura wake wawe na amani kwani yupo tayari kuwa mtumishi wao wa kuwasemea changamoto wanazopitia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Mtia nia huyo anataja mambo ya kuyavalia njuga ni pamoja na kuhakikisha ujenzi wa barabara nyingi za jimbo hilo kwa kiwango cha lami.

“Kwa muda mrefu eneo la Kivule limesahaulika katika masuala mengi ikiwamo uchakavu wa miundombinu ya barabara, hili utabaini unapofika maeneo haya barabara zake huwezi amini kama za moja ya maeneo ya Dar es Salaam kwa sababu kwa muda mrefu hakukuwa na mtu sahihi wa kuwasemea Bungeni changamoto wanazokabiliana nazo.

“Wana-KIvule wakinichagua hawatajutia uamuzi wao, nitahakikisha barabara zinajengwa katika kiwango cha lami.

Nasema hivi kwa sababu mar azote baada ya mvua kuisha barabara nyingi za jimbo la Kivule zimebaki mahandaki, serikali inachofanya kutia vifusi kipindi cha masika mashimo yanarudi tena.

Pikipiki ikipita kwa tabu barabara ya Msongola- Kivule ambayo miundombinu yake  siyo rafiki kwa matumizi.

.........................................

“Wananchi wa Kivule ni watu tuliosahaulika kwa muda mrefu kama maandiko yanavyosema kila jambo na wakati wake na kila ufalme ni wa Mbingu, wakati huu nimejawa na nia ya kuomba mnichague nikawasemee changamoto tunazopitia, maeneo mengine yanahatarisha hadi afya za wagonjwa hasa kinamama wajawazito na waliojifungua,” anasema.

Jambo jingine analozungumzia kulikomesha ni rushwa katika shule za sekondari na msingi.

“Ukienda kwenye shule nyingi za msingi na sekondari za serikali kuomba umhamishie mtoto wako nje ya ofisi ya mwalimu mkuu kuna karatasi imeandikwa “Hakuna nafasi za kuhamia  wanafunzi”.

“Unapoingia kwa mkuu naye atakuthibitishia hilo, ukitoka siku ya pili mwingine atakuambia mtoto wake amemhamishia hapo, nafasi amepataje amempa rushwa mkuu wa shule au mwalimu mkuu.

“Kumbe nafasi zinatolewa kwa rushwa, nikichaguliwa nitalivalia njuga jambo hilo na kulikomesha kabisa,” anasema Marwa.

Hata hivyo, ameahidi kutoa sehemu ya mshahara wake kuhakikisha wanafunzi wanapata mlo kamili shuleni ili kuwawezesha kujifunza vizuri kutokana na shibe.

“Nikichaguliwa nitahakikisha wanafunzi wanakula shuleni, na hilo litafanikiwa baada ya kuwashirikisha wazazi na walimu, name mwenye nitatoa sehemu ya mshahara wangu ‘kusapoti’kufanikisha jambo hilo,” anasema Marwa.

Kuhusu sekta ya afya anasema Serikali imelekeza watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano na wazee wasiojiweza wahudumiwe bure katika hospitali za serikali huku wazee nao

wapatiwe huduma mara moja lakini hilo halitekelezwi kutokana na kukosekana usimamizi.

“Nitahakikisha katika hospitali, zahanati na kwenye vituo vyetu vya afya hilo linazingatiwa ili kuondoa mataka miongoni mwa wanajamii,” anasema.

Vitendo vya rushwa kwa kiasi kikubwa wahanga ni jamii lakini maskini ni waathiriwa wakubwa zaidi kwa sababu wanawanyimwa haki ya kupata huduma wanastahili kwa wakati.

Anasema pamoja na mambo mengine atahakikisha maeneo ya kutolea huduma za afya, elimu na ofisi za umma anakomesha vitendo rushwa vilivyokithiri ambavyo vinawanyima haki za kupata huduma zao hususan walio maskini.

Marwa anasema tatizo la uhaba mkubwa wa maji safi litabaki historia kwa sababu atajikita katika kuhakikisha wapiga kura wake wanapata maji safi na salama kwa kunywa na mtumizi mengine ya nyumbani.

Piki iki ya magurudumu matatu ikipita kwenye barabara hiyo ambapo mgombea huyo wa ubunge anasema iwapo akichaguliwa itakuwa ndiyo kipaumbele chake namba moja kuitengeneza.

................................

Anafafanua hilo atalifanikisha kwa kuwasilisha kero hizo katika kuwasilisha kero hizo bungeni lakini pia kutafuta wafadhili mbalimbali watakaosaidia kumaliza jambo hilo.

Changamoto nyingine na atahakikisha maeneo yote yasiyo na umeme yanafikiwa na huduma hiyo muhimu ya nishati, lakini pia atawekea mkazo wananchi wake kujenga makazi bora kwa

ajili ya kuishi.

Mchakato wa kupitisha wagombea ili wakapigiwe kura na wananchi ili kupitishwa jina mgombe mmoja kwa chama husika kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), limekamilika na Agosti nne watapigiwa kura.

No comments