VYOMBO VYA HABARI VYAASWA KULINDA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI
Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka
Na Kelvin Kijo
TUME Huru Uchaguzi ya Taifa (INEC) itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari na kuhakikisha wananchi wanapata taarifa kwa wakati katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhani wakati akiwasilisha mada katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
"INEC tutaendelea kushirikiana na wanahabari wazalishaji wa maudhui mitandaoni ili kuhakikisha walaji taarifa sahihi na kwa wakati, “ alisema Ramadhani
“Tunaamini vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuhakikisha uchaguzi mchakato wa unafanyika kwa amani hivyo tunaviomba vyombo vya habari kuhakikisha habari zinazotolewa zinazingatia maadili na kuepuka Maudhui yanayoweza kuchochea chuki au ghasia,” alisema Kailima.
Mwakilishi wa Shule Kuu ya Uandishi wa habari wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IJMC), Dkt. Egbert Mkoko amesema wahariri na waandishi wa vyombo vya habari vya umma na binafsi wanapaswa kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi ili kuepusha taarifa za kutenganisha taifa.
“vyombo vya habari vinapaswa kutoa habari za ukweli zisizo na ubaguzi wa aina yoyote” alisema Dkt Mkoko.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Utangazaji Mamalaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Andrew Kisaka aliwaasa waandishi na wahariri kuepuka kusambaza taarifa za uwongo ambazo zinaweza kuchochea migogoro.
“Toeni vipaumbele kwa sauti zinazoshawishi amani kwa umma na kurejesha utu wa kitanzania kuhusu dhana potofu kuhusu upinzani wao wa kisiasa na mchakato wa uchaguzi” alisema Kisaka.
Aidha katika kuangazia uchapishaji wa taarifa binafsi za watu Mkuu wa Mawasiliano Serikalini katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Innocent Mungi ametoa rai kwa wahariri na waandishi wa habari ya kuepuka kuandika taarifa za uchochezi.
“Kuweni na sera za kushughulikia maswala ya faragha na taarifa binafsi na kuwaweka wazi walengwa kufahamu namna taarifa zao zitakavyotumiwa,”. alisema Mungi.
Ameongezea kuwa matumizi ya teknolojia na akili mnemba yatumiwe kwa utashi wa mhariri awe ndio final decision maker wa habari.
Mwakilishi wa Tume Huru ya Uchaguzi INEC, Mtibora Selemani amewataka wahariri na waandishi wa vyombo vya habari kuelewa taratibu za Uchaguzi kabla, wakati na baada ya Uchaguzi na kujua wajibu wao bila kuathiri mchakato wa Uchaguzi.
Mkuu wa Mawasiliano Serikalini katika Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC) Innocent Mungi, akichangia jambo.
Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhani akizungumza.
Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhani akiteta jambo na mmoja wa maafisa wa Tume hiyo ya uchaguzi.
Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi a washiriki.
Mwakilishi wa Shule Kuu ya Uandishi Wa habari wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (IJMC), Dkt. Egbert Mkoko akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
No comments