SIKU NNE ZA MATESO WODINI MZEE HUYU, ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU
Ana miaka 68, amekwisha katwa kidole, yupo Temeke Hospitali hajui hatima yake
Anachangamoto ya kutosikia, zinatakiwa Sh.220, 000 ili afanyiwe kipimo cha CT-SCAN.
Mahitaji mengine ya kibinadamu ni changamoto.
Wasamaria wema wanaomsaidia waomba msaada zaidi wa watanzania.
Mzee Said Bakari Nyumbu (68), akiwa nyumba anayoishi.
............................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
Mzee Said Bakari Nyumbu (68) Mkazi wa Mtaa wa
Ngurungu , Maji Matitu (A) Mbagala Jijini Dar es Salaam maisha yake yako
hatarini kufuatia maradhi yanayomsibu na sasa anaomba msaada wa Sh. 220,000 ili
afanyiwe kipimo cha CT-SCAN aendelee na matibabu.
Mzee huyo ana siku ya nne sasa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke kwa
matibabu lakini yupo katika wakati mgumu kutokana na kutokuwa na uwezo wa
kifedha zaidi ya kuwategemea wasamaria wema ambao wamelazimika kuwaomba watanzania
kujitokeza kumsaidia mzee huyo ili kuokoa maisha yake.
Mzee huyo anachangamoto ya kutosia,
amekatwa kidole cha mguuni lakini kutokana na kuathirika zaidi mguu wake madaktari
wamemuambia anatakiwa afanyiwe kipimo cha CT-SCAN kuanzia kiuoni hadi miguuni
ili kuona kama atakuwa ameathirika zaidi baada ya kujichoma na kitu chenye ncha
kali katika kidole kilichokatwa alipokuwa kwenye miangaiko yake ya kujitafutia
riziki.
Hali ya mzee huyo siyo nzuri
kutokana na maisha duni aliyonayo na maradhi yanamsumbua.
Mbali ya kukatwa mguu pia anatakiwa
kufanyiwa upasuaji wa tezi dume lakini ameshindwa kufanyiwa baada ya kukosa Sh.
700,000 za kufanyiwa upasuaji.
Ndugu watanzania hizo ndiyo shida anazopitia
mzee wetu huyu, anaomba msaada wa hali na mali ili aweze kupata fedha za
kumsaidia kupata matibabu na fedha za kujikimu.
Kama utaguswa kumsaidia unaweza
kuwasiliana na Mzee Ally Abdallah Ngurungu na pia Mjumbe wa Shina namba Nne Mwajuma Mshana
ambao wanamsaidia kwa namba ya simu 0784679755 (Ally Abdallah Ngurungu) au
Mwandishi wa Taarifa hii kwa namba 0754362990 kwa maelezo zaidi.
Ndugu Watanzania kwa kiasi chochote
cha fedha utakacho jaaliwa na Mwenyezi Mungu iwe Sh. 1000, 2000, 5000 na zaidi
ya hapo ukitoa zitamsaidia mzee huyu ambaye hajui hatima ya maisha yake na
jambo kubwa zipatikane fedha za kipimo hicho cha CT-SCAN zinazohitajika. Kutoa ni
moyo na Mungu atakubariki kwa utoaji wako.
Shime watanzania kwa umoja wetu tushikamane
kumsaidia mzee wetu Saidi Nyumbu kuokoa maisha yake.
Changamoto ya ugonjwa ya Mzee Saidi Nyumbu imeibuliwa na Wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Matitu A kupitia CCM, ikiwa ni moja ya njia ya kutatua changamoto za wananchi wajumbe hao ni Hawa Omari na Jihadi Umwagala.
Mzee Said Bakari Nyumbu (68) akiwa na Mzee Ally Abdallah Ngurungu (kushoto), ambaye wamekuwa wakimsaidia na wasamaria wema.
No comments