TUME HURU YA UCHAGUZI YAKABIDHI FOMU ZA UTEUZI KWA MGOMBEA URAIS WA CCM
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan. Mgombea huyo wa CCM amechukua fomu hizo leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na mgombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama hicho, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi wakionesha mkoba wenye fomu za kuomba uteuzi wa nafasi hizo baada ya kukabidhiwa leo Agosti 9,2025 ambapo Tume inataraji kufanya uteuzi Agosti 27 mwaka huu.
No comments