MADEREVA BODABODA NA BAJAJI WILAYA YA MBOZI WAMKARIBISHA RC MAKAME, WAMUAHIDI KULINDA AMANI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame akizungumza na madereva bajaji, bodaboda na maguta walioshiriki Jogging iliyoandaliwa na Maafisa usafirishaji wilayani Mbozi iliyofanyika Agosti 9, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo. Maafisa usafirishaji walitumia Jogging hiyo kumkaribisha mkuu huyu wa mkoa baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza mkoa huo.
.................................................
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
ILIKUWA Jogging ya kihistoria iliyowakusanya makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo madereva bodaboda na bajaji Wilaya ya Mbozi ikiwa na lengo la kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri O. Makame wilayani humo huku wakiahidi kuwa mabalozi wa kulinda amani hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.
Jogging hiyo iliyofana iliandaliwa na vijana waenda bodaboda na bajaji yenye lengo la kumkaribisha Mhe. Makame ambapo wamesema wanaishukuru serikali kwa kuendelea kutambua mchango wao.
Pia, wamesisitiza kuwa wataendelea kuwa mabalozi wa kuhamaisha amani katika jamii wakati wa utendaji kazi wao.
Katibu wa waendesha bajaji Wilaya ya Mbozi, Abel Mwambene amesema kuwa Serikali ya Mkoa wa Songwe imeendelea kuyatambua makundi hayo kwa kuwashirikisha mambo mengi yanayoigusa jamii.
Mhe. Makame ameshukuru kwa mapokezi hayo akieleza kuwa Serikali ya inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassana ina imani kubwa na mchango wa vijana katika kuleta maendeleo huku Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Hammad Mbega akisema kuwa Wilaya ya Mbozi itaendelea kuwa salama muda wote.
Maafisa Usafirishaji wa MMkoa wa Songwe (katikati walioshika mbuzi) wakimkabidhi kitoweo hicho mkuu wa mkoa huo Jabir Omary Makame kwa ajili ya kumpa Rais Samia Suluhu ili apate supu ikiwa ni kumpongeza baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais.Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega akisisitiza jambo baada ya kushiriki jogging na maafisa usafirishaji wa mkoa wa Songwe.
Mazoezi mbalimbali yakifanyika wakati wa Jogging hiyo.
Mazoezi yakiendelea kufanyika.
Mazoezi yakiendelea.
Mazoezi yakiendelea. 'Hapa ni kanyaga twende'
Mazoezi yakipamba moto. Kutoka kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omary Makame, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholas Livingstone.
No comments