Breaking News

MADEREVA BODABODA WILAYA YA MBOZI WAMPA RAIS SAMIA MBUZI WA SUPU BAADA YA KUCHUKUA FOMU YA URAIS

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame  akizungumza na  madereva bajaji,  bodaboda na maguta walioshiriki Jogging iliyoandaliwa na Maafisa usafirishaji wilayani Mbozi iliyofanyika Agosti 9, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.

.................................................

Na Mwandishi Wetu, Songwe.

MADEREVA bajaji, bodaboda na maguta Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wamemzawadia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mbuzi kwaajili ya supu atakayotumia baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais.

Mbuzi hiyo iliyotolewa na Madereva Pikipiki za miguu mitatu (bajaji) na miwili (Bodaboda) na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Songwe Jabir Omary Makame  leo Agosti 9, 2025 katika Jogging iliyoandaliwa na Maafisa usafirishaji wilayani Mbozi Mkoani Songwe.


Wakizungumza na Makundi mbalimbali Madereva wamedai wamefikia hatua hiyo baada ya kupewa mikopo ya asilimia 10 yaliyobadili maisha yao, pia wameahidi kutokuwa kikwazo katika uchaguzi kwa kukwepa mihemho inayoweza kusababisha vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani.


Akizungumza baada ya kukabidhiawa mbuzi hiyo, RC Makame  amewaagiza Mamlaka ya Usafiri Ardhini Latra Mkoa wa  Songwe kuacha tabia ya kukusanya ushuru kwa kuwakimbiza badala yake watumie vingozi wa makundi hayo.


Maafisa Usafirishaji wa MMkoa wa Songwe (katikati walioshika mbuzi) wakimkabidhi kitoweo hicho mkuu wa mkoa huo Jabir Omary Makame kwa ajili ya kumpa Rais Samia Suluhu ili apate supu ikiwa ni kumpongeza baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega akisisitiza jambo baada ya kushiriki jogging na maafisa usafirishaji wa mkoa wa Songwe.
Mazoezi mbalimbali yakifanyika wakati wa Jogging hiyo.
Mazoezi yakiendelea kufanyika.
Mazoezi yakiendelea

Mazoezi yakiendelea.

Mazoezi yakiendelea. 'Hapa ni kanyaga twende'
Mazoezi yakipamba moto. Kutoka kushoto mwenye miwani ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Omary Makame, Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Hamad Mbega na Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Nicholas Livingstone.
 

No comments