WANDISHI WA HABARI WASISITIZWA KUZINGATIA ULINZI, USALAMA KAZINI
Hayo yamejiri katika semina fupi ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari mkoa wa Singida yaliofanyika katika ofisi za klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida (SINGPRESS) ambapo zaidi takribani waandishi wa habari 18 wameshiriki semina hiyo.
Akizungumza mwezeshaji wa semina hiyo Jamaldini Abuu ambaye ni mwandishi wa habari aliyejengewa uwezo na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kwa kushirikiana na (IMS) amesema mwandishi wa habari akiwa salama basi habari anazoandika zitakuwa salama kwa maslahi ya jamii
“Usalama wa Mwandishi unaanza na Mwandishi mwenyewe hivyo ni jukumu la kila Mwandishi kuzingatia usalama wake akiwa kazini kabla ya kazi, wakati wa kazi na hata baada ya kazi husika” alisema.
Aidha amewataka waandishi wa habari kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao akisema ndio vitakuwa nguzo kuu ya kulindana na kusaidiana hasa zinapotokea changamoto za kiusalama kwa waandishi zinazoweza kuathiri utendaji kazi wao.
Kwa upande wake Mshiriki wa semina hiyo Edina Malekela amesema mafunzo hayo yamemuwezesha kutambua baadhi ya vitu ambavyo vimemfumbua macho hasa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuhakikisha anakuwa salama na kujua mipaka yake kama mwandishi itakayolinda usalama wake.
“Binafsi kuna vitu nilikuwa sivijui lakini kupitia mafunzo hayo nimeweza kuelewa kwamba kunavitu vya msingi sana kama mwandishi napaswa kuvizingatia katika utekelezaji wangu wa majukumu”
Ameongeza kuwa katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu anapaswa kuzingatia zaidi usalama wake kwanza kuliko kazi anayoenda kuifanya ambayo inaweza kuhatarisha usalama wake.
Nae Abdul Ramadhani amesema wao kama vijana mafunzo hayo yamewafungua na kuwapa mwanga mkubwa katika kujikinga wao wenyenwe na vifaa vyao pamoja muonekano wao ambao utaweza kuwapa utambulisho chanya katika jamii.
“Tumepata uwelewa mkubwa sana, tumejua namna ya matumizi sahihi ya vifaa vyetu tunavyovifanyia kazi kila siku na namna ambavyo tunaweza kujikinga tukiwa katika shughuli zetu za kila siku za uandishi wa habari namna ambavyo tunaweza kutengeneza muonekano wetu.
Licha ya kuwashukuru wawezeshaji wa mafunzo hayo ambao ni Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) ameomba mafunzo ya namna hayo yawe ni mwendelezo hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu kwakuwa tasnia ya habari ni mtambuka.
Elikana Obeid amesena tasnia ya habari ni nyeti katika jamii inayohitaji umakini katika utendaji wake jambo ambalo mafunzo hayo yaliyotolewa yatawarahisishia kufanya kazi zao kwa ufasini zaidi ili kuwa salama na kuepuka rungu la sheria.
Mafunzo hayo yanatolewa chini ya mradi wa Empowering Journalists for Informed Community (Kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili jamii iweze kupata taarifa) unaotekelezwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na (IMS) ambapo miongoni mwa maeneo ya mradi huo ni kuhusu masuala la ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari, usalana wa mwandishi wa Habari Mtandanoni na Digital Safety Training and Tackling Online Gender-Based Violence for women journalists.Mafunzo yakiendelea.
Mwanahabari Jamaldini Abuu wa Mkoa wa Singida, akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo hayo.
Mwanahabari Jamaldini Abuu wa Mkoa wa Singida, akionesha fulana ambayo anaweza kuvaa mwandishi anapokuwa kwenye shughuli zake ili kutambulika.
Mafunzo yakifanyika.
Mafunzo yakiendelea.
Picha ya pamoja.
No comments