WATUMISHI WA TARURA DODOMA WAPATA MAFUNZO YA UKIMWI, UVV NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA MAHALA PA KAZI
Mtaalam akimchukua vipimo mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.
...........................................
Na Godwini Myovela, Dodoma
WATUMISHI wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dodoma Wameshiriki mafunzo ya Ukimwi, VVU na magojwa yasiyoambukizwa mahala pa kazi. Zoezi hili la mafunzo limeenda sambamba na upimaji wa afya kwenye upande wa magonjwa ya homa ya ini, VVU na UKIMWI, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya Taasisi kwa kila robo.
Katika ufunguzi wa zoezi mafunzo na upimaji Meneja wa Mkoa, Mhandisi Edward Lemelo aliwaeleza watumishi umuhimu wa afya bora mahala pa kazi kwani itachangia kuwa na matokeo chanya kwenye utekelezaji wao wa majukumu ya kila siku. Pia itawasaidia watumishi kujitambua mapema endapo wana changamoto za kiafya na kuanza kuchukua hatua kabla ya matatizo kuwa makubwa.
aliwasihi watumishi kutumia mafunzo kwa usitawi wa afya bora mahala pa kazi. Sambamba na hayo alitoa Shukurani zao za dhati kwa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana nao katika Zoezi hilo.
Baada Zoezi la mafunzo na upimaji kuhitimishwa Mratibu wa Mafunzo kwa niaba ya Meneja wa mkoa, Bi. Ana Semkiwa, alisema lengo kuu ni kuhakikisha watumishi wanabaki na afya bora ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Bw. Gideoni Julius, Mtaalamu wa Maabara kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, alisema changamoto za afya bado ni kubwa kwa jamii na hivyo upimaji wa mara kwa mara unasaidia kuokoa maisha.
“Tunawahimiza watumishi na wananchi wote kwa ujumla kuondoa hofu na kuendelea kupima afya zao mara kwa mara, kwani kujua hali yako ni hatua ya kwanza ya kujilinda na kulinda wengine,” alisema Julius.
Mmoja wa washiriki, Bi. Agatha Mayaya, alisema zoezi hilo limewasaidia kupata elimu na uelewa mpana juu ya afya na kuongeza ari ya utendaji kazini.
“Tunaishukuru ofisi ya meneja wa TARURA Dodoma kwa uratibu mzuri na pia wataalamu wa afya kwa huduma waliyoitoa, maana imekuwa fursa muhimu ya kujitambua kiafya na kuongeza umakini wetu kazini,” alisema Mayaya.
Wataalam wakiwa kwenye mafunzo hayoMafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo.
No comments