Breaking News

WAZEE WA TAASISI YA TANGA ASILI WAPONGEZA USHINDI WA DKT. SAMIA

 Wazee wa 'Tanga Asili' wapongeza ushindi wa Rais Dkt Samia.

 Waahidi kushirikiana na Serikali bega kwa bega.

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Wazee wa Tanga  (TANGA ASILI), Mohamed Ali Dondo akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa pongezi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa kuwa Rais.Kushoto ni Mweka Hazina wa Taasisi hiyo, Mohamed Hussein Kassanali na kulia ni Mkamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Hamza Makame..

..................................................

Na Mwandishi Wetu, Tanga.

TAASISI ya Wazee ya Wilaya ya Tanga(TANGA ASILI), imempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ushindi mkubwa alioupta kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Oktoba 29 mwaka huu, matokeo yaliyoelezwa kuwa yamedhihirisha mapenzi waliyonayo wananchi dhidi ya Serikali yao.

Kwa niaba ya taasisi ya Tanga Asili, Katibu  Mkuu wake Mohamed Ali Dondo, katika mkutano na wanahabari mkoani Tanga, amempongeza Rais huyo wa Jamhuri ya muungano na Makamu wake Dkt Emmanuel Nchimbi pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Aidha Dondo alisema kuwa, ushindi huo wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ymewafanya wananchi kujawa na imani kubwa juu ya kupata mabadiliko makubwa kwenye suala zima la uharakishwaji wa maendeleo yao.

‘‘ Kwa niaba ya Tanga Asili tunamtakia maisha marefu na afya njema, tukiamini awamu hii kutakuwa na mabadiliko makubwa katika maendeleo ya wananchi’’ alisema Dondo.

Pamoja na hayo,Dondo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Salha Burian na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kusimamia vyema mchakato mzima wa uchaguzi Mkuu tangu pale ulipoanza hadi ulipoweza kuhitimishwa.

Dondo alisemma lengo la taasisi hiyo ni kuhakikisha inarejesha hadhi ya Mkoa wa Tanga kama ambavyo ilikuwa imeasisiwa na wazee wa nyakati zilizopita ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Wajumbe wa Taasisi hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea
Mjumbe wa Wazee Asili, Mohamed Dhikri akitoa ufafanuzi kwa Waandishi wa habari kwa baadhi ya mambo yaliyojiri kwenye kikao hicho cha wazee.
 

No comments