Breaking News

DKT. SAMIA AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa iliyoketi jijini Dodoma, leo Jumatano, Novemba 5, 2025. 

Kikao hicho pamoja na Mambo mengine kimefanya uteuzi wa  wagombea wa nafasi za  Spika na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  pamoja na nafasi ya Spika na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao hicho.

Kikao hicho kikiendelea. 

No comments