KIFO CHA SALEHE IDD: FAMILIA YAMWACHIA MUNGU
Dada wa marehemu, Asha Idd, akizungumza na waandishi wa habari.
.................................
Na Onesmo Kapinga.BAADA ya kifo cha mkazi wa Zavala, Kata ya Buyuni, Ilala jijini Dar es Salaam, Salehe Idd, familia imesema kwamba inamwachia Mungu kutokana na tukio hilo.
Marehemu Salehe alifariki Desemba 4, mwaka akiwa njiani kwenda hospitali ya Amana, Dar es Salaam.
Ikidaiwa marehemu alichomwa kisu usiku wa alfajiri nyumbani kwake kabla ya kupeleka hospitali ya Nguvu Kazi iliyoko Chanika.
Baadaye, marehemu Salehe alifariki wakati akielekea Amana kwa ajili ya matibabu zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari, mtoto wa kwanza wa kiume wa marehemu, At human Salehe alisema baada ya kupata taarifa ya tukio hilo, alifika hospitali ya Nguvu Kazi na kumkuta baba yake akiwa amekata kauli.
Athuman alisema kutokana na tukio hilo, msimamo wa familia wanamwachia Mungu kwa sababu hawafahamu mtu aliyehusika na tukio hilo.
"Sisi kama familia tunamwachia Mungu kwa sababu hatujui aliyetenda tukio la kumchoma kisu baba yetu," alisema Athuman
Alisema pamoja na mambo mengi yanasemwa mitaani, lakini wao kama familia, wanachukulia tayari wamemzika baba yao na tukio limepita.
Naye, Dada ya marehemu, Asha Idd alisema pamoja na kifo cha kaka kinaudhinisha, kwa namna kilivyotokea, lakini tukio hilo limepita.
Asha ambaye anaishi Magore, alisema mpaka sasa hawamjui mtu aliyehusika na tukio hilo na anayelijua ni Mwenyezi Mungu.
"Baada ya kupigiwa simu nilifika Hospitali na kumkuta kaka yangu amefariki baada ya ya kuchomwa kisu na mtu ambaye bado hajajulikana na tayari tumekwisha mzika na tukio sasa limekwisha pita," alisema Asha.
Kwa upande wake Ally Athuman ambaye ni mpwa wa marehemu aliungana na familia na kueleza kuwa jambo hilo wanamuachia Mungu muweza wa yote.





.jpg)




No comments