Breaking News

NAIBU SPIKA KUTOA USHIRIKIANO KWA MADIWANI BABATI DC

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mheshimiwa Daniel Sillo akizungumza katika hafla ya kuapishwa kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Desemba 3, 2025.

.....................................

Na Mwandishi Wetu, Babati

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mheshimiwa Daniel Sillo, ameshiriki zoezi la kuapishwa kwa madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati  Desemba 3, 2025.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mheshimiwa Sillo amewataka madiwani kutimiza wajibu wao kwa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu na kujituma, huku akiahidi kushirikiana nao katika kila hatua ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo yanayostahili.

Aidha, amewasisitiza madiwani kuwa wabunifu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyoiwezesha halmashauri kupata fedha zaidi za kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Sillo pia amewakumbusha madiwani kutembelea wananchi mara kwa mara katika kata zao ili kusikiliza changamoto, kutoa mrejesho wa utekelezaji wa shughuli za halmashauri na kuimarisha uwakilishi wao.

No comments