Breaking News

DC KILOSA AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Waziri Mkuu wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba akiwasili na ujumbe maalumu kukagua athari za mvua wilayani Kilosa Mkoa wa Morogoro. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka.

.................................... 

Ameandika Cde Shaka  Hamdu Shaka DC Kilosa

Tunamshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuma ujumbe maalum wake ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mwigulu Nchemba  kufika wilayani kwetu (Kilosa) Mkoa wa Morogoro.

Pamoja na mambo  mengine alikagua athari zilizotokana na mvua na kutoa faraja na maelekezo kufuatia janga la mafuriko lililopelekea kuharibu miundombinu ya reli na barabara na kusababisha changamoto ya usafiri na usafirishaji.

Athari zilizotokea ni pamoja na kaya 140 zenye idadi ya wakaazi 501 kupoteza makazi yao, kaya 408 kuharibikiwa na maeneo yao ya maakazi na wananchi watano kupoteza maisha kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.

#DktSamiampangomzima 

#kaziututunasongambele

No comments