KHAMBAY MBUNGE MWENYE SHUKURANI, MAONO
......................
Na Dotto Mwaibale
Uongozi ni mamlaka ya kuwaonyesha watu njia kwa
vitendo ni dhana au taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa
kuwawezesha wale wanaongozwa naye kuunganisha nguvu na vipaji vyao na kuvitumia
ili kufikia malengo ya maendeleo.
Bora
kiongozi ni kiongozi ambaye anafanya kazi bila ya kushirikiana na wananchi anachoamua ndicho anataka kifuatwe hana muda
wa kuwaelezea mipango ya kazi.
Hata
anapofanyiwa jambo zuri hajui kutoa shukurani anaona alistahili kufanyiwa hivyo
yakiwemo mambo mengine yanayofanana na
hayo.
Mbunge wa Jimbo
la Babati Mjini Mhe Emmanuel Khambay ni kiongozi bora mwenye maono kwa jinsi
anavyoshirikiana na wananchi na viongozi wenzake mbalimbali kuhakikisha wana
Babati wanapata maendeleo.
Khambay ni
mtu wa watu kiongozi anayejua kushukuru, wakati wote walipo wananchi kwenye
shughuli za maendeleo, furaha na huzuni hakosekani.
Mhe. Khambay
Januari 4,2026 alishiriki kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Babati Mjini ambapo alitumia fursa hiyo kuwashukuru
wajumbe wa kikao hicho kwa niaba ya wananchi kwa ushindi uliokipata chama hicho
katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Aidha,
katika kikao hicho alitoa taarifa ya kazi mbalimbali alizozifanya baada ya kula
kiapo cha ubunge ambapo aliomba kuendelea kupewa ushirikiano ili aweze kutekeleza
miradi ya maendeleo iliyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025/
2030. Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mhe. Emmanuel Khambay,, akiwashukuru wajumbe wa kikao hicho.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye kikao hicho.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea
Mbunge Khambay akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Diwani Viti Maalumu Wilaya ya Babati Mjini, Salome Masasi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mhe. Yona Wao na kulia Mwakilishi wa CCM.
Taarifa hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale 0754362990
Chanzo (Nick- Studio)





.jpg)




No comments