Muonekano wa mashimo ya migodi katika maeneo ya uchimbaji wa madini
................................................................
Na Mwandishi Wetu, Simiyu
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu zaidi ya
21 wamefariki dunia kufuatia ajali ya kufunikwa na ardhi katika Mgodi wa
Ng'alita, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.
Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea baada ya
kudaiwa kuingia mgodini kwa kujipenyeza kinyume cha sheria kwani shughuli za
uchimbaji zilikuwa zimesitishwa.
Kufuatia ajali hiyo iliyotokea saa 11 alfajiri
Januari 13,2024 , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa
zao katika ajali hiyo na kwamba Vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na
uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama
ndani ya kifusi. |
No comments