Breaking News

RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR


 ....................

Na Dotto Mwaibale

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kuitwa Wanawake na Muungano yatafanyika Aprili 25, 2024 Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi ambapo wananchi wamealikwa kwenye siku hiyo maalumu ya kumbukizi ya maadhimisho hayo ya  Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

No comments