Breaking News

MBUNGE SUMA FYANDOMO AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUSHUSHA BEI YA MBOLEA

Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) Mkoa wa Mbeya Mhe. Suma Fyandomo akichangia katika bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni Dodoma Mei 5, 2024

..............................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Mbeya Mhe. Suma Fyandomo amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha za ruzuku kutoka mfuko wa  mbolea wa kilo 50 uliokuwa unauzwa kwa Sh. 150,000 ukashuka bei mpaka  Sh. 60,000 NA sh. 70,000

Fyandomo alitoa pongezi hizo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo Bungeni Dodoma Mei 5, 2024

"Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na Amir Jeshi Mkuu kwa kazi kubwa nzuri ambayo aliwaona wakulima maana walikuwa kwenye kipindi kigumu sana ambapo Mbolea ilikuwa na bei kubwa sana lakini Rais aliweza kutoa fedha za ruzuku kutoka Mfuko wa Mbolea wa Kilo 50 uliokuwa unauzwa kwa Tsh. 150,000 ukashuka bei mpaka Tsh. 60,000 mpaka Tsh. 70,000," - alisema Mbunge Fyandomo.

Fyandomo alisema Bajeti aliyosoma Mhe. Hussein Bashe kuomba na ikapitishwa ya Tsh. Trilioni 1.2 ninaiunga mkono kwa asilimia Mia Moja. Nakupongeza Mhe. Hussein Bashe kwa kusimamia afya za watoto wetu kwa kufuatilia virutubisho vya Mchele ulioingizwa nchini kutoka Marekani.

"Wilaya ya Rungwe, wananchi wengi wanategemea kilimo cha Chai, kuna Kiwanda cha Chai cha Chivante ambacho kimefungwa ambapo kuna wananchi wa Kayuki, Nsekela, Katonya, Ruwarisi, Ndende na Kiganga wananchi wote wana Chai za kutosha. Mhe. Hussein Bashe kaangalie kile Kiwanda wananchi wakichuma Chai wanaipeleka wapi?" alihoji Mbunge Fyandomo.

Alisema  wakulima wa Chai waliopo Wilaya ya Rungwe ambao wanapeleka Chai kwenye Kiwanda cha Chai cha Katumba ambao wapo maeneo ya Rungwe, Kapugi, Masebe, Sekela, Mwakaleli, Mamo, Lopa, Itete, Kimo, Suma na Nditu Wanafanya vizuri lakini  hawapati fedha kwa wakati.

Fyandomo alisema mwaka 2022 Serikali iliahidi Mufindi, Iringa kujenga Kiwanda cha kuchakata Maparachichi, eneo limepatikana na Kiwanda ni cha kusaidia wananchi wa Nyanda za Juu Kusini ikiwemo Njombe, Mbeya, Iringa, Songwe. Tukuyu, Rungwe ambao wamejikita  kupanda maparachichi baada ya kusikia kauli ya Serikali. Tunaomba Waziri utuambie ni lini Kiwanda kitaanza kujengwa," Mbunge Fyandomo aliomba jibu hilo wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Kilimo.

Mbunge Fyandomo alisema Wilaya ya Mbarali na Kyela zilitolewa Sh. Bilioni 79 kwa ajili ya Skimu za Umwagiliaji ambapo alimuomba Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kwa kumueleza kuwa Mkoa wa Mbeya una Wilaya za  Mbeya DC, Busokelo, Chunya, Rungwe ambazo zinahitaji  Skimu za Umwagiliaji na kuwa na kuwa makundi ya  Wanawake na Vijana wanajituma kufanya kilimo kwa kuwa ndiyo kazi yao kubwa wanayoitegemea kuwainua kiuchumi.

No comments