Breaking News

KIONGOZI MBIO ZA MWENGE : JAMII TOENI TAARIFA ZA UNYANYASAJI KWENYE VYOMBO VINAVYOHUSIKA

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akimkabidhi Mwanafunzi mwenye mahitaji vitu mbalimbali wakati alipotembelea banda la wanafunzi hao Mwenge wa Uhuru ulipokuwa kwenye mbio za kukagua miradi ya maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Julai 5, 2024.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Na Dotto Mwaibale, Itigi

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava ameiomba jamii panapokuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji na ukati wa kijinsia kutoa taarifa kwa vyombo husika ili hatua ziweze kuchuliwa.

Mnzava alitoa ombi hilo wilayani Itigi mkoani Singida Julai 5, 2024 wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Halmashauri ya wilaya hiyo  vyenye thamani ya zaidi ya  Sh.Milioni 1 kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye mahitaji wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea banda la watoto kwenye mbio zake za kukagua miradi ya maendeleo na kuweka jiwe la msingi na  baadhi kuizindua.

Alisema mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji si la mtu mmoja bali ni la wote na ndio maana Rais Samia Suluhu Hassan aliunda wizara inayoshughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia.

Mnzava alisema Rais hakuishia kwa kuanzisha wizara hiyo tu bali ameenda mbali zaidi kwa kuelekeza kila yanapojengwa majengo ni lazima ihakikishwe inajengwa miundombinu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.

Aidha kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 alisema mbali ya kujenga majengo yenye miundombinu rafiki kwa watu wenye uhitaji Rais Samia amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu kwa kundi hilo na kuwa huo ndio utashi wa Serikali kwa kutambua changamoto hizo na kuchukua hatua ya kizitatua.

Mnzava alisema katika jamii tuliyopo kuna changamoto kwani  baadhi ya watu wamekuwa wakiwabagua, kuwanyanyapaa na hata kuwafanyia vitendo vya kikatili ambavyo vingine inakuwa vigumu hata kuvieleza.

Alisema Serikali haikuwa tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea kufanyika na akatumia nafasi hiyo kutoa wito kwa jamii pale inapoona kuna vitendo hivyo vinafanyika watoe taarifa polisi, ofisi za ustawi wa jamii na maeneo mengine yanayohusika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu  hao.

Katika hatua nyingine Mnzava aliridhia miradi yote sita iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani humo kwa kuikagua, kuweka jiwe la msingi na kuizindua huku kukiwa hakuna mradi hata mmoja ambao umekataliwa.

Akizungumzia miradi ambayo ilikuwa na kasoro ndogondogo aliomba ifanyiwe marekebisho haraka iwezekanavyo ili iweze kutumika kwa walengwa ambao ni wananchi na akataka itunzwe ili iweze kudumu kwa muda mrefu ikizingatiwa kuwa Serikali kupitia Rais Samia imetoa fedha nyingi kuikamilisha.

Miradi iliyotembelewa na Mbio za  Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 4 ni wa Maji uliopo eneo la Mabondeni, Mradi  ujenzi wa  Shule ya Sekondari Majengo, Hospitali ya Wilaya uliowekewa jiwe la msingi, mradi wa barabara ya lami nyepesi ya mita 600, kugawa vifaa kwa watu wenye mahitaji maalumu, mradi wa vijana na  mradi wa huduma za jamii, ujenzi wa kituo cha TTCL

Miradi yote hiyo imetembelea na kukaguliwa, kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 chini ya kauli mbio isemayo  “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akimkabidhi mwanafunzi mwingine vitu hivyo.
Mwanafunzi mwenye ulemavu akikabidhiwa miguu ya bandia ya kutembelea
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Majengo wakikabidhiwa taulo za kike na mmoja ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akipima ubora wa sakafu katika Shule ya Sekondari ya Majengo. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akikagua Barabara ya Msikitini yenye urefu wa mita 600.Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota akizungumza kabla ya kumkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, kuweka jiwe la msingi Barabara ya Msikitini. 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Klabu ya Kupinga Rushwa Shule ya Sekondari Majengo George Yohana baada ya kuifungua klabu hiyo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari ya Majengo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Kemirembe Lwota.
Wanafunzi wa Halaiki wakione ukakamavu wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Itigi.
Mwalimu John Jackson wa Shule ya Msingi Mlowa akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kuwa wakakamavu.
Muonekano wa jengo la Utawala la Shule ya Sekondari ya Majengo lililowekewa jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akimkabidhi 
Wanafunzi wakiwa katika mapokezi ya Mwenge mjini Itigi.
Wanawake na Mama Samia wa Wilaya ya Manyoni wakiwa kwenye mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Itigi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akiangalia igizo la kupinga rushwa wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa lililooneshwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Majengo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akipanda mti aina ya Jacaranda mbele ya jengo la Utawala la Shule ya Sekondari Majengo.

Muonekano wa Jengo la Mkonga wa Taifa la Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ambalo lilikaguliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, lilijengwa wilayani Itigi.
Meneja wa TTCL MMkoa wa Singida, Augustino Mwakyembe (kushoto)b akitoa maelezo ya ujenzi wa jengo hilo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava
Muonekano wa moja ya jengo la Hospitali ya Wilaya ya Itigi ambalo liliwekwa jiwe la msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, akipatiwa maelezo ya mradi wa Barabara ya Msikitini ya mita 600 kabla ya kuwekwa jiwe la msingi.
Wanafunzi wakiwa kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi Barabara ya Msikitini.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Kemirembe Lwota, akimuomba Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, kukagua na kuweka jiwe la Msingi mradi wa Barabara ya Msikitini. 
Wananchi wakiwa Stendi ya Zamani ya Itigi ambapo Mwenge wa Uhuru 2024 ulikesha.
 

No comments