MWILI WA MAREHEMU MEJA JENERALI CHARLES MBUGE (MSTAAFU) WAAGWA NYUMBANI KWAKE TABATA SEGEREA
Askari wa eshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) nyumbani kwake Tabata Segerea jana Oktoba 15, 2024 baada ya kumalizika kwa zoezi la kuuaga..
…………………
Na Mwandishi Wetu, Dar
es Salaam
MNADHIMU Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman, amewaongoza familia na waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Meja Jenerali Charles Mbuge (Mstaafu) nyumbani kwake Tabata Segerea jana Oktoba 15, 2024.
Mwili wa marehemu, Meja Jenerali Charles Mbuge (mstaafu) unatarajiwa kuagwa kijeshi Oktoba 16, 2024 katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baada ya taratibu za kuagwa kijeshi kukamilika, Mwili huo utasafirishwa kuelekea mkoani Mara kwa mazishi yatakayofanyika Oktoba 17, 2024.
Baadhi ya watu wamemuelezea mareheme Mbuge kwa ujapakazi wake na kuwa alikuwa akipendwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Pombe Magufuli kwa uchajikazi wake na usimamizi wake wa miradi ikiwemo ujenzi wa ukuta Mererani, Msingi wa Ikulu Chamwino na bado alikamilisha ujenzi wa nyumba za Ukonga (quartes ) ,alikuwa mtiifu, Mzalendo na mwanamapinduzi wa kweli hivyo atakumbukwa na kuenziwa kwa dhati.
Jeneza lenye mwili wa marehemu, Meja Jenerali Charles Mbuge (mstaafu) likiwa kwenye gari maalumu la JWTZ.
Ndugu, Jamaa na marafiki wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Meja Jenerali Charles Mbuge
Heshima za mwisho zikitolewa.
Utulivu ukitamalaki wakati wa zoezi la utoaji wa heshima za mwisho kwa marehemu.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa limebebwa.
No comments