RAIS MWINYI: SMZ IMEWEKEZA KATIKA MIUNDOMBINU YA AFYA
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akizungumza na Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Dunia (Global Fund), Dk. Sara Asiimwe, na ujumbe wake ulioongozwa na Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui.
.............................
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali imewekeza kwa
kiwango kikubwa katika miundombinu ya afya kutokana na umuhimu wa sekta hiyo
kwa jamii.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 15 Oktoba
2024, Ikulu, Zanzibar, alipokutana na Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Dunia
(Global Fund), Dk. Sara Asiimwe, na ujumbe wake ulioongozwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar ,
Nassor Ahmed Mazrui.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameishukuru “Global Fund”
kwa jitihada zake za kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa
kuisaidia kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo sekta ya afya.
Halikadhalika, Rais Dk. Mwinyi amepongeza juhudi
za “Global Fund” za kuisaidia Zanzibar katika sekta ya afya na nyingine za
maendeleo, akisisitiza kuwa zinasaidia jitihada za Serikali anayoiongoza katika
kutekeleza azma ya kutoa huduma bora za afya.
Akizungumzia huduma ya bima ya afya kwa wageni
wanaoingia Zanzibar, Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali ina dhamira ya
kuanzisha bima hiyo kutokana na umuhimu wake kwa wageni, hivyo ameomba Mfuko
huo uangalie namna ya kuiunga mkono Serikali.
Naye, Dk. Sara Asiimwe alimueleza Rais Dk. Mwinyi
kuwa “Global Fund” inafanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kupitia sekta zake za maendeleo, ikiwemo Wizara ya Afya. Aidha,
aliahidi kuwa taasisi yao itaendeleza ushirikiano na Zanzibar, hasa katika
miradi ya maendeleo.
Mazungumzo yakiendelea
Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Dunia (Global Fund), Dk. Sara Asiimwe, akizungumza.
Waziri wa Afya wa Zanzibar , Nassor Ahmed Mazrui. akizungumza kwenye kikao hicho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi na Meneja Mwandamizi wa Mfuko wa Dunia (Global Fund), Dk. Sara Asiimwe (katikati) , na ujumbe wake ulioongozwa na Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kufanyika kwa kikao Ikulu Zanzibar.









.jpg)




No comments