Breaking News

MAKALLA: MSIWACHAGUE WAPINZANI HAWAAMINIANI NA HAWAAMINIKI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, akihutubia katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kata ya Manzese, Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, Novemba 24, 2024.

.................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
 

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla amesema vyama vya upinzani haviaminiki, wala viongozi wao hawaaminiani, hivyo wagombea wake hawastahili kuchaguliwa.

Makala amesema hayo wakati akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, katika Kata ya Manzese, Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Novemba 2024.

Makalla alitoa wito kwa wananchi kuwachagua wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika kesho kutwa.

Makalla alisema vyama hivyo vya upinzani haviwezi kuaminiwa kupewa nafasi ya kuongoza mitaa, vijiji wala vitongoji, kwa sababu viongozi wake hawana uadilifu.

"Hela tu ya majimbo walikuwa wanatafuna hawa ndiyo uwape mitaa hiyo mihuri itakuwa salama?

"Hawaaminiki wa lolote na wao wenyewe hawajiamini. Mwaka 2020 walipata wabunge 19 wa viti maalum, lakini wakawatimua, mna uhakika gani hawa wenyeviti wakichaguliwa kama hawatawatimua?," alihoji Makalla.

No comments