USIKU WA GUMI LA DHAHABU' WATIKISA PANGANI.
Na Mashaka Kibaya.
MKUU wa
Wilaya ya Pangani Gift Msuya ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha mchezo
wa ngumi unakwenda kuipaisha wilaya hiyo na kuitangaza kitaifa na hata katika
medani za Kimataifa.
MKUU huyo
ametoa Kauli hiyo jana (02/11/2024) alipokuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la
mchezo wa ngumi lililopewa jina la usiku wa 'Gumi la dhahabu', pambano ambalo
limefanyika katika ukumbi wa Pangadeco Beach Hotel.
Wilaya ya
Pangani kupitia Pangani Boxing Promotion
imeendesha mpambano huo wa ngumi za ridhaa kwa lengo la kuhamasisha
Wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa
ifikapo Novemba 27 mwaka huu.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi wa mchezo huo,Mkuu huyo wa wilaya Gift Msuya,alisema
kwamba atashirikiana na ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaaa Hamidu Aweso
kuibua na kulea vipaji na hivyo vijana wanaocheza mchezo huo kufika kwenye
medani za Kimataifa.
"Tunataka
wageni waje kujifunza Pangani na tupate vipaji tutakavyovipeleka Duniani na
Pangani iweze kujulikana zaidi.Washindi tutawapromoti waende kushindana
mashindano ya Kitaifa na Kimataifa ili kwenda kuonesha vipaji vyao na
kuitangaza Pangani yetu" alisema Mkuu wa Wilaya.
Tamasha hilo
la ngumi lilikuwa na mapambano Tisa (9) yaliyowashirikisha Vijana mabondia wa
Wilaya ya Pangani na wale wa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga ambao waliweza
kuibuka kidedea licha ya wenyeji ambao walioonekana kuwa wachanga kwenye
masumbwi kuweza kutoa upinzania mkali.
Aidha Mkuu
wa Wilaya Gift Msuya amemtaja Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwamba Kiongozi
mwenye upendo kwenye sekta ya michezo ambaye amekuwa akifanya hamasa kubwa ya
kuwazawadia wanamichezo.
"Rais
Dkt Samia hoyeee... hapa unajua kwanini nini nimemtaja.Ni kwa sababu amekuwa
akifanya makubwa hasa kutoa hamasa kwenye michezo anatoa fedha nyingi.Hata leo
nilikuwa napitia 'comment' social media comment ya kwanza ya kwake juu ya Azam
kuifunga Tanga hapa anadhihirisha timu zote ni zake"alisema DC Gift.
Katika
mpambano huo DC Gift alichangia Shilingi 500,000 kwa Pangani Boxing Talent
waandaji wa tamasha hilo la ndondi ili kuwawezesha kufanikisha mchezo huo ambao
wahusika walimueleza kukabiliwa na ukata wa fedha.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya Gift Msuya alitumia fursa hiyo kuwahimiza Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kupiga Kura hapo Novemba 27 mwaka huu alisema,hiyo ni hatua muhimu katika kuwapata viongozi kwa ajili ya kusimamia maendeleo yao.
No comments