MASAUNI : BIASHARA YA KABONI BI UKOMBOZI KWA TAIFA
Atembelea kituo cha Taifa cha ufuatiliaji Morogoro.
DC Shaka Morogoro imejipanga na iko tayari kutumia fursa.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema kituo cha Taifa cha ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) nchini kilichopo Mkoani Morogoro kitakuwa ni miongoni mwa taasisi muhimu nchini katika kusaidia Taifa kutokana na miradi mbali mbali ambayo mataifa ya nje yanakuja kuwekeza kupitia biashara ya Kaboni, ili biashara hiyo iweze kusaidia katika kukuza kipato cha wananchi lakini pia kuchangia uchumi wa nchi kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kutembelea kituo
hicho kilichopo mkoani Morogoro.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka ambae alimuwakilisha Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro katika ziara hiyo
amesema mkoa huo umejipanga kutumia vyema fursa hiyo ili kutekeleza na
kutafsiri kwa vitendo maelekezo na maono
ya Rais Samia ya kuhakikisha biashara ya
Kaboni inakuwa vyenzo vyengine ya kuinua kipato cha wananchi na kuchangia
katika maendeleo nchini.
"Ni fursa muhimu sana kwetu uwepo wa kituo hiki mkoani
kwetu ni hatua muhimu sana, kwani vianzio vyote vinavyopelekea biashara hii
kufanyika tunavyo kupitia misitu, mifugo na
mito tutahakikisha fursa hii inatumika vyema na tija iweze kuonekana kwa
wananchi na Taifa kwa ujumla kupitia rasilimali tulizonazo," alisema Shaka.
No comments