RC DAR ES SALAAM AZINDUA TUMAINI JEMA GROUP
Afisa Tawala Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila wakati wa hafla ya uzinduzi wa Tumaini Jema Group (TJG) iliyofanyika Februari 11, 2025
.....................................
Na Dotto
Mwaibale, Dar es Salaam
MKUU wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amezindua rasmi Tumaini Jema
Group (TJG) linalohusisha mitaa minne ya Liwiti, Amani, Mfaume na Misewe lililopo Tarafa ya Ukonga
Kata ya Liwiti Tabata Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Afisa Tawala Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja
akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa
kikundi hicho cha Kijamii iliyofanyika Februari 11, 2025 alisema ni cha muhimu
sana kwani kimejikita zaidi kujiinua kiuchumi.
Alisema
uanzishwaji wa kikundi hicho unaunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
za kuwainua kiuchumi ambaye anaangaika kutafuta fursa za kiuchumi ndani na nje
ya nchi na kueleza kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam itaendelea
kuwapa ushirikiano.
Mgonja
aliwataka wanakikundi hicho kuchangangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa
na halmashauri kwa wanawake, vijana, walemavu na makundi mengine hasa
ikizingatiwa kuwa wana usajili wa Serikali.
Mgonja
aliwapongeza wana kikundi hicho kwa kutunza hali ya usalama na utulivu nchini
kwani bila ya amani hakuna kinachoweza kufanyika ambapo alitumia nafasi hiyo
kuwaomba wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2025 utakapo wadia
wampe kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti
wa Kikundi hicho, Deogratias Kajula akizungumzia historia fupi ya kikundi hicho
alisema wazo la kukianzisha liliibuliwa
baada ya jirani yao mmoja kufariki na familia yake haikuwa na kipato cha
kutosha kukidhi gharama za mazishi hivyo majirani walilazimika kushirikiana na
familia kwa njia mbalimbali ili kuweza kumsitili marehemu.
Alisema wazo
hilo liliweza kupata mashiko katika mitaa miwili ya Misewe na Liwiti ambapo
wananchi wa mitaa hiyo walilipokea kwa mikono miwili na ndipo hatua za
kutengeneza rasimu ya katiba ilipoanza.
Katibu wa
Kikundi hicho, Stanley Mmanyi alisema malengo ya Tumaini Jema Group ni kushirikiana
kijamii katika shida na raha, kushirikiana kiuchumi na kujiletea maendeleo
akielezea suala la kusaidiana katika shida na raha ni kutembeleana na kujuliana hali
hususan misiba na ugonjwa kwa mwanakikundi.
Akizungumzia
kuhusu raha alisema ni kusaidiana na mwanakikundi iwapo atakuwa anaoa au
kuolewa hama kuozesha na kuinuana kiuchumi kwa
nia ya kujiletea maendeleo.
Mmanyi akitaja malengo mengine ya kikundi hicho kuwa ni pamoja na kuwekeza
kwenye mifuko mbalimbali kama vile UTT-Amis,
mabenki ya biashara, kukusanya maduhuli na tozo za Halmashauri mbalimbali zilizoko
katika Mkoa wa Dar es Salaam kama vile kukusanya ushuru wa masoko,
minada ya Halmashauri kwa makubaliano maalumu na halmashauri husika.
“ Ombi letu kubwa tunaomba tusaidiwe kulinunua shamba lililopo Vibula Kifuru Hali ya Hewa la Bi Hilda Machumu Bigambo lenye ukubwa wa Ekari 6.0 lenye thamani ya Sh.Milioni 200 na katika kutekeleza miradi yote tunayotarajia kuifanya tunahitaji kuwa na jumla ya Sh. Milioni 232.8,” alisemma Mmanyi.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Deogratias Kajula akitoa taarifa kwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo. |
Mgeni rasmi akisaini kitabu cha wageni baada ya kuzindua kikundi hicho.
Viongozi mbalimbali wa Tumaini Jema Group wakiwa kwenye uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Leopord Duma, Godbless Mushi, Stanley Mmanyi, Deogratias Kajula, Gabriel Maleko na Anyisile Kyoso.
Hafla hiyo ikiendelea. Kutoka kushoto ni Stella Babu, Atuganile Kabalika na Lameck Chotta.
Furaha ikitamalaki kwenye uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Taswira ya uzinduzi huo.
Uzinduzi ukiendelea.
Mwenyekiti wa kamati ya hafla hiyo, Anyisile Kyoso akifurahi na Katibu wa Kikundi hicho, Stanley Mmanyi.
Ni furaha tupu kwenye uzinduzi huo.
Maafisa wa Benki ya NMB kutoka Tawi la Mandela, wakishiriki katoka uzinduzi huo ambapo walipata fursa ya kutangaza bidhaa zao. Kutoka kushoto ni Afisa Mauzo wa benki hiyo, Miraji Selestin, Afisa Bima wa benki hiyo, Mariam Godfrey na Afisa Mauzo, Deo Makuru.
Wajumbe wa Kikundi hicho wakifuatilia matukio mbalimbali. Kutoka kushoto ni Mzee Godwini Mwambande na Dennis Mlatie.
Furaha ikitawala kwenye uzinduzi huo.
Afisa Mauzo wa benki hiyo, Miraji Selestin, akizungumza. Kulia ni Afisa Mauzo wa benki hiyo tawi la Mandela, Deo Makuru.
Taswira ya uzinduzi huo.
Group Menager wa Tanzania Commercial Bank, Neema Lutatenekwa (kulia) akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alizinadi bidhaa za benki hiyo. Wengine ni Wafanyakazi wa benki hiyo.
Hafla ikiendelea. Wajumbe wa Kikundi hicho wakiwa na vipeperushi vya bidhaa mbalimbali za Tanzania Commercial Bank,
Furaha ikitamalaki wakati wa kumpokea mgeni rasmi.
Afisa Tawala Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Flora Mgonja, akiongoza wajumbe kuserebuka kufurahia uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Upendo Cartering & Decoration ambao waliandaa chakula cha kiwango cha hali ya juu katika uzinduzi huo wakiwajibika. Kwa mahitaji ya huduma yao piga simu namba 0788364010 au 0767663967 wanapatikana Tabata Liwiti jijini Dar es Salaam.
No comments