VYOMBO VYA UTANGAZAJI VYATAKIWA KUSIMAMIA HAKI NA USAWA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU 2025
Wazizi wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa watoa huduma za Utangazaji 2025 wa siku mbili ambao umeanza leo Februari 13 hadi 14, 2025 jijini Dodoma.
..................................
Na Dotto Mwaibale, Dodoma
VYOMBO vya Utangazaji nchini vimetakiwa
kusimamia haki na usawa na haki katika kuhabarisha taifa mwenendo wa
kampeni za vyama vya siasa pamoja na kuzingatia weledi na kanuni za utangazaji.
Ombi hilo limetolewa na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi wakati
akifungua mkutano mkuu wa watoa huduma za Utangazaji 2025 ulioanza leo Februari
13 na kufikia tamati kesho Februari 14, 2025 jijini Dodoma.
“Nitoe rai kwa washiriki
wote wa mkutano huu kuhakikisha kuwa mnazielewa sheria na kanuni zote
zinazosimamia uchaguzi mkuu nchini,” alisema Kabudi.
Alisema ni marajio yake
kuona mada zote zitakazowasilishwa kwenye mkutano huo zitalenga
kukumbushana wajibu wa vyombo vya Utangazaji kuelekea uchaguzi mkuu
ili wananchi waweze kuelimika na kufanya maamuzi sahihi katika kipindi
cha uchaguzi.
Kabudi alisema Sekta ya
Utangazaji nchini na duniani kote imekumbwa na mabadiliko ya kiteknolojia
ambayo yamefanya vyombo vya utangazaji wa kijadi kuathiriwa kwa kiwango
kikubwa kwenye uwekezaji walioufanya.
Alisema Serikali
inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufanyia kazi
changamoto mbalimbali zinapitiwa na vyombo vya utangazaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambao ndio waandaaji wa
mkutano huo, Dkt. Jabiri Bakari alisema wameboresha sana eneo la
huduma kwa wateja na kuwa kwenye kila kanda kuna mameneja na lengo lao ni kukua
zaidi ili waweze kusonga mbele.
Alisema jambo lingine ni kuwa wanafanya kazi hiyo ili
waendelee kufanya vizuri na kwa ustadi mkubwa ambapo alitoa shukurani kwa
washiriki wa mkutano huo kwa michango yao.
Alisema Tanzania ni nchi yetu na kuwa vyombo vya habari vya
mataifa ya wenzetu ya nje vimekuwa vikiandika habari za kizalendo zaidi kwa
maslahi ya nchi zao .
“Teknolojia imeturahisishia kufanya kazi vizuri na kuchangia
maendeleo makubwa ya kiuchumi lakini pale taarifa zinapokuwa na changamoto ni
vizuri kuliangalia jambo hilo kwa maslahi ya nchi yetu,” alisema Dkt. Bakari
Dkt. Bakari aliomba kutumia simu za mkononi kwa ajili ya
kufanya mambo ya maendeleo badala ya kuzitumia tofauti jambo ambalo linaweza
kuturudisha nyuma.
Mtoa mada kwenye mkutano huo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma, Mhadhiri
Abdallah Katunzi akizungumzia dhima ya vyombo vya habari vya utangazaji alisema
ni kutetea maslahi ya umma, kusimamia amani na usalama wa nchi na kuwa ni gundi
ya kushikanisha umoja wa nchi yetu.
Aidha, Katunzi alisema waandishi wa habari katika kipindi cha
uchaguzi wanatakiwa kuandaa agenda mahususi badala ya kutegemea zaidi viongozi
waliopo madarakani. Aliongeza kwamba sauti za wananchi ni muhimu sana
kujumuishwa kwenye kazi za waandishi wa habari wakati wa uchaguzi.
“Mara nyingi sauti za wananchi wa kawaida imekuwa ni ndogo
kutokana na waandishi kutowahoji na kutoa kipaumbele zaidi kwa wagombea,”
alisema Katunzi.
Alisema katika kipindi hicho cha uchaguzi wagombea wanaume
taarifa zao zimekuwa zikiandikwa zaidi kuliko za wagombea wanawake.
Washiriki wa mkutano huo wakichangia mijadala suala kubwa
lililoibuka ni wanatasnia ya habari waliowengi hawana elimu ya kutosha na suala
zima la kiuchumi nalo limetajwa kuchangia kufanya kazi pasipo kufuata kanuni na
sheria.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali, Geryson Msigwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, akizungumza kwenye mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui TCRA, Saida Muki, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria wa Tume Huru ya Uchaguzi (INEC), Cyprian Mbugano akitoa mada kuhusu Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.Washiriki wa mkutano huo kutoka Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamojaBloggers wakiwa katika majadiliano ya tathimini ya utekelezaji wa maadhimio ya mkutano mkuu wa utangazaji wa mwaka 2024.
Taswira ya mkutano huo.
Washiriki wakiwa katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Meneja wa Redio Harvest Time FM, Getson Sanga na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Misalaba Media ya Mkoa wa Shinyanga, Mapuli Misalaba.
Washiriki kutoka Tanzania Blogger Network (TBN) wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa.
Mkutano ukiendelea.
WWaendeshaji wa Online TV wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mkutano huo wakijisajili kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Washiriki wakibadilishana mawazo wakati wa mkutano huo.
Mkutano ukiendelea. Kutoka kushoto ni Kinara Lafuli kutoka Singida, Imani Ponera kutoka Site Digital, Edina Malecela kutoka Singidani Online TV na Mkurugenzi Mtendaji wa Cales Digital, Cales Katemana.
Mhariri Mtendaji wa Tanganyika Online TV, Hadia Khamis (kushoto) akiwa na Mhariri wa SM TV, Magreth Mkiga.
Taswira ya mkutano huo.
Mkutano ukiendelea. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Nicco Media TV, Mwandishi wa Habari wa Jambo Tv, Theophil Mbunda na Mkurugenzi wa Habari Faster, Emmy Mwaipopo.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia bada zilizokuwa zikitolewa.
Mwanahabari Mkongwe, Abdallah Majula akichangia jambo kwenye mkutano huo.
No comments