SHAKA : UIMARA WA RAIS SAMIA NI MATOKEO CHANYA YA UONGOZI UNAOJALI KESHO YA NCHI
Asifu Mapinduzi makubwa sekta ya mawasiliano na internet.
Abainisha Mapinduzi ya ukombozi kupitia SGR na bwawa la Nyeyeree
Awapongeza Vodacom kwa kufikisha vituo 456 vya huduma nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu akikata utepe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogo wakati wa uzinduzi wa Duka la 456 Huduma kwa wateja kupitia kampuni ya simu ya Vodacom katika Kituo cha SGR (Jakaya Mrisho Kikwete Station)
Na Mwandishi wetu Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema uimara wa Rais Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake ni matokeo chanya, unaojali kesho ya Nchi yetu (vizazi vya leo na kesho) kwa kukamilisha mradi wa kimkakati wa SGR kutoka Dar - Morogoro - Dodoma.
Amefahamisha kuwa kukamilika kwa mradi huo kumerahisisha usafiri miongoni kwa wananchi baina ya morogoro na mikoa jirani ambako kumechochea biashara na shughuli nyingine za kiuchumi na kijamii kuimarika na kukua kwa kiwango kikubwa.
Ameyasema hayo katika kituo cha SGR (Jakaya Mrisho Kikwete Station) wakati *akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika uzinduzi wa Duka la 456 Huduma kwa wateja kupitia kampuni ya simu ya Vodacom katika kituo hicho.
'Ufanisi wa mradi huu ni matokeo ya kukamilika kwa mradi wa umeme wa Bwawa la Mwl Nyerere ambao umekamilishwa na Rais Samia. Mradi huo umetupa uhakika wa umeme kwa ajili ya uendeshaji wa mradi huu wa SGR huu ni ukumbozi mkubwa katika sekta ya usafiri na usafiri haji sambamba na upatikanaji wa nishati ya umeme kwa uhakika" alisema.
Amefahamisha kuwa watanzania wameendelea kushuhudia mapinduzi makubwa katika sekta ya mawasiliano ya simu na intaneti nchini ambapo serikali ya Rais Samia imeendelea kujenga mazingira rafiki na wezeshi kwa makampuni ya mawasiliano kama Vodacom na wengine kuwekeza na kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi.
"Tusione vyaelea vimeundwa na muundaji mwenyewe ni Jemedari Rais Samia. Matokeo makubwa ya utendaji kazi wake katika kipindi cha miaka minne ya usimamizi wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020 - 2025 yanawapa wapinga maendeleo kiwewe nanyi pia mashuhuda"
"Niwaambie vitendo vina sauti kuliko maneno matupu. Matokeo ya kazi kubwa na nzuri ya maendeleo na uimarishaji wa huduma kwa wananchi yanamfanya Rais Samia aishi kwenye mioyo na akili za watanzania walio wengi na hiyo ndio sababu wapinga maendeleo wanapata hofu kabla ya muda, watulie Rais Samia bado ana kazi ya kukamilisha" alisema.
Hata hivyo Shaka aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa uamuzi wa kutumia fursa hiyo kuwekeza katika kituo hicho, kuwahudumia watanzania na wageni mbalimbali watakaosafiri na SGR pamoja na wananchi wa maeneo ya jirani, hatua inayotoa nafasi pia kwa Watanzania kuwa sehemu ya mabadiliko ya kidijitali.
Mkurugenzi wa Mauzo na Usambazaji vodacom, George Rugata alisema kuwa
vodacom itaendelea kutoa huduma za kisiasa ambazo sio tu kuwarahisihia wananchi
kupata huduma kwa urahisi lakini pia kuinua maisha ya wananchi na kuimarisha
uchumi nchini ambapo jumla vituo 456 vimefunguliwa katika mikoa mbali mbali
nchini.Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu akizungumza wakati wa ufunguzi wa kituo hicho.
No comments