DKT BITEKO : MALENGO YA MATUMIZI NISHATI SAFI YA KUPIKIA HAYAWEZI KUFIKIWA BILA YA MWANAMKE
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko (kulia) akipata maelezo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia alipotembelea mabanda wakati wa kongamano la kuhamadisha matumizi ya nishati hiyo lililoandaliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
............................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko,
amesema, matumizi ya nishati safi ya kupikia hayawezi kufikiwa malengo bila
kumshirikisha mwanamke.
Dkt. Biteko amesema hayo wakati wa kongamano la kuhamadisha matumizi
ya nishati safi ya kupikia lililoandaliwa na TANESCO kuelekea maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa machi 8 kila mwaka.
Amesema ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia
inatekelezeka, na amewataka wanawake wote nchini kumuunga mkono rais Dkt Samia
Suluhu Hassan ili kufikiwa yifikapo 2034 watu wote hususani wanawake wote
nchini wawe wanatumia nishati safi ya kupikia kwa umeme.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga amesema Serikali imetia mkazo katika
matumizi ya nishati safi ya kupikia na ni gharama nafuu na rahisi kwa matumizi.
Pia amesema lengo limelenga kuhakikisha Kila mwanamke wa
Tanzania anapata fursa ya kutumia nishati safi ya kupikia kwa umeme.
Maelezo ya matumizi ya nishati safi ya kupikia yakitolewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Gissima Nyamo- Hanga akizungumza.
No comments