P0LISI NIGERIA YAWATIA MBARONI WAISLAMU 20 KWA KULA MCHANA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
..................................................
Na Mwandishi Wetu
IKIWA ni siku ya tatu tangu Waislamu wakiwa wameanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Polisi wa Kiislamu katika jimbo la Kano, kaskazini mwa
Nigeria wamewakamata Waislamu 20 waliokutwa wakila mchana hadharani wakati wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan ambapo pia Watu watano wamekamatwa kwa kuuza chakula
huku Naibu kamanda wa Polisi Mujahid Aminudeen akisisitiza kuwa msako huo
utaendelea mwezi mzima.
Aminudeen amesema hatua hiyo inalenga kudumisha heshima ya
Ramadhan kwani Waislamu wanapaswa kufunga kuanzia alfajiri hadi jua linapozama
pia ameeleza kuwa wale waliokamatwa tayari wamefikishwa katika Mahakama ya
Sharia kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mbali na hilo Polisi wa kiisalmu wa Hisbah pia wamewakamata
Watu waliovaa mavazi yanayokiuka maadili ya Kiislamu wakiwemo waliokuwa na
nywele zisizoruhusiwa na Madereva wa Bajaji waliowachanganya Abiria wa jinsia
tofauti.
Mfumo wa Sharia umeendelea kutumika katika baadhi ya majimbo ya kaskazini mwa Nigeria kwa Waislamu tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka 20 iliyopita na kutoa adhabu kwa wale wanaokiuka na kukamatwa wakila hakula mwezi mtukufu.
No comments