MHANDISI TIA SINGIDA : WANAFUNZI TUMIENI FURSA YA UJENZI MRADI WA JENGO LA TAALUMA KUFANYA VIBARUA
Mhandisi TIA Singida, Godfrey Seni akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Tasisi hiyo.
..............................
Na Dotto Mwaibale, Singida
MHANDISI wa
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida, Godfrey Seni amewataka
wanafunzi wa Taasisi hiyo kutumia muda wao wa mapumziko kufanya vibarua katika
mradi wa ujenzi wa jengo la taaluma ili kujipatia fedha za kujikimu chuoni
hapo.
Seni
aliyasema hayo wakati akizungumza na Wanafunzi wa mwaka wa kwanza ambao
wanaanza msimu wa masomo wa 2025/ 2026 ‘Orientasion for First Year Students’ katika
kikao kilichofanyika Novemba 20, 2025.
“Wanafunzi
katika chuo chetu kuna mradi ambayo unafanyika baada ya Serikali kutupa fedha
nawaombeni mnapokuwa kwenye mapumziko baada ya masomo njooni kufanya vibarua ili
muweze kujipatia fedha za kuwasaidia badala ya kwenda kuzurura mitaani,”
alisema Seni.
Seni
aliwaambia wanafunzi hao kuwa katika kampasi hiyo Serikali imetoa fedha Sh.
Bilioni 13.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la taaluma hivyo watumie fursa hiyo
kwa kufanya vibarua na kujipatia fedha jambo litakalo wasaidia wazazi wao wasiangaike
kuwatafutia fedha za matumizi.
Alisema
jengo hilo litakuwa la ghorofa tano likiwa na kumbi za mihadhara, madarasa,
kumbi za mikutano pamoja na ofisi na hadi kukamilika litatumia Sh. Bilioni 16.
Katika hatua
nyingine Seni aliwataka wanafunzi hao kuitunza miundombinu mbalimbali iliyopo
chuoni hapo ili iweze kudumu na wanafunzi wengine waje waikute kama walivyo
ikuta.Wanafunzi wakimsikiliza Mhandisi wa TIA Kampasi ya Singida, Godfrey Seni.





.jpg)




No comments