UKOSEFU WA UWAJIBIKAJI CHANZO CHA RUSHWA YA NGONO VYUONI
...........................
Na Dotto
Mwaibale, Singida
UKOSEFU wa
Uwajibikaji na Uwazi katika Mifumo ya Chuo imeelezwa kuwa ni sababu za kuwapo
kwa rushwa ya ngono Vyuoni.
Hayo
yameelezwa na Afisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa
Singida, Benjamini Masyaga wakati akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza
wa msimu wa masomo 2025/ 2026 ‘Orientation for first year
students’ katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Singida Novemba
19, 2025.
“ Pale ambapo hakuna ufuatiliaji wa walimu,
taratibu za alama hazipo wazi, au mawasiliano kati ya wanafunzi na uongozi ni
dhaifu, rushwa ya ngono hujitokeza kwa wingi,” alisema Masyaga.
Alisema Vyuo vinaposhindwa kuwaadhibu hadharani
wahusika, mazingira yanayotia moyo rushwa ya ngono huendelea.
Masyaga alitaja sababu nyingine inayofanya
vitendo vya rushwa ya ngono iendelee ni baadhi ya wahalifu kurudi vyuoni baada
ya kuhamishwa bila adhabu.
Alitaja sababu nyingine ni ile ya ushawishi
kwani baadhi ya wanafunzi hasa wanaoingia chuo kwa mara ya kwanza, huathiriwa
na marafiki wanaoona ngono kama njia ya kupata msaada, hivyo kupunguza uwezo wa
kutambua ukatili au rushwa.
Masyaga alisema ili kuzuia na kupambana na
rushwa ya ngono inatakiwa Elimu na Uhamasishaji kwa wanafunzi itolewe kupitia
warsha za mara kwa mara.
Alieleza jambo lingine ni kuwepo kwa uadilifu
wa kitaaluma, haki na wajibu wa mwanafunzi na namna ya kuiripoti rushwa ya
ngono pamoja na kuanzisha kozi fupi za Ethics and Anti- Corruption kw wanafunzi
wapya (Orientation)
Afisa huyo wa Takukuru alitaja baadhi ya njia
nyingine za kupambana na rushwa ya ngono ni kuimarisha mfumo wa uongozi na
usimamizi wa chuo kwa kuanzisha taratibu za wazi na shirikishi katika utoaji wa
alama, usajili, malazi, udahili, mitihani na huduma nyingine.
Alisema matumizi ya mfumo wa kidijitali (online
systems) unasaidia kupunguza mwingiliano wa ana kwa ana unaowez kuchochea
rushwa.
Alitaja njia nyingine kuwa ni kuanzishwa na
kuimarisha Dawati la Malalamiko kwa chuo husika kuwa na dawati huru ambalo
litapokea taarifa bila ya kuvuja na wanafunzi wapewe njia salama za kuripoti na
kuweka kanuni za kulinda mtoa taarifa.
Aidha, Masyaga alisema Serikali ya Wanafunzi
iwe na mafunzo ya maadili, uwajibikaji na uongozi bora na kuweka mifumo ya
uwazi katika matumizi ya fedha za wanafunzi na miradi ya serikali hiyo. Wanafunzi wa mwaka wa kwanza TIA Singida wakisikiliza mada iliyohusu rushwa ya ngono vyuoni iliyokuwa ikitolewa na Afisa wa Takukuru, Benjamini Masyaga,





.jpg)




No comments