WANAFUNZI: TAASISI YA UHASIBU SINGIDA MAHALI PAZURI KUPATA ELIMU
.......................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya
Uhasibu Tanzania (TIA), Kampasi ya Singida imetajwa kuwa ni mahali pazuri
kupata elimu kutokana na kozi mbalimbali zinazotolewa na maboresho mazuri ya
miundombinu.
Hayo
yamebainishwa na Emmanuel Marko Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza ngazi ya cheti wa
Taasisi hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
‘Orientasion for First Year Students’ iliyofanyika Novemba 20, 2025.
“Niwaombe wazazi
na walezi wawalete watoto wao kuja kupata mafunzo ya kozi mbalimbali kwenye
chuo hiki kwani ni mahali sahihi pa kupata elimu itakayo wasaidia katika maisha
yao,” alisema Marko.
Aidha, Marko
alisema chuo hicho kina mazingira mazuri ya kujifunzia walimu na wafanyakazi
wake chini ya Mkurugenzi wa Kampasi hii Dkt. James Mrema ni wakarimu wamewapokea
vizuri hivyo wanatoa shukurani zao kwao.
Marko
alisema tangu walipofika baada ya chuo hicho kufunguliwa kwa ajili ya msimu wa
masomo wa mwaka 2025/ 2026 wameelekezwa mambo kadha wa kadha kama kuwa na
nidhamu na kutojihusisha na vitendo mbalimbali ambavyo haviendani na maadili.
Alivitaja
baadhi ya vitendo hivyo kuvaa mavazi yasiyo na staha ya kubana miili yao wakati
wakiwa chuoni na maeneo mengine nje ya chuo, kuvaa fulana, kofia aina kapero,
kaptura au suruali chini ya makalio ‘Kata K’ na kunyoa kiduku.
Aliyaeleza mambo
mengine walioelekezwa ni kutojihusisha na vitendo vya mahusiano ya kimapenzi,
uvutaji wa bangi, kutoka chuoni bila ya ruhusa na kusisitiziwa kuzingatia
masomo wakati wote kwani ndilo jambo ambalo limewapeleka chuoni hapo na si
vinginevyo.
Marko
alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika chuo hicho
ambacho kinatoa fursa ya kupata elimu kwa watoto na makundi mengine ya
watanzania.
Kwa upande
wake Rais wa Serikali ya Wanafunzi (TAISO), Maiba Loitare
amewasisitizia wanafunzi hao kuzingatia masomo na kufuata taratibu na sheria za
chuo.
Aidha,
aliupongeza uongozi wa kampasi hiyo kwa kuweka utaratibu wa kutoa matangazo
Stendi Kuu ya Mabasi ya Mkoa wa Singida Misuna kwa ajili ya kuwaelekeza
wanafunzi wageni namna ya kufika katika chuo hicho bila ya kupata usumbufu.
Loitare aliipongeza Serikali
kwa kuboresha miundombinu ya chuo hicho na kukifanya kuwa sehemu ya mvuto
kupata masomo kwani imeipatia taasisi hiyo Sh. Bilioni 13. 5 kwa ajili
ya ujenzi wa jengo la taaluma ambao ujenzi wake unaendelea kwa kasi chini ya
Mkurugenzi wa TIA Singida Dkt. James Mrema.
Afisa
Utumishi na Msimamizi wa Huduma za Rasilimali Watu na Utawala wa Taasisi hiyo,
Sanura Mohamed akizungumza na wanafunzi hao aliwaambia taratibu zote za namna ya kufanya wakiwa
chuoni hapo zimeweka bayana ili kila mwanachuo azielewe hivyo ni wajibu wao
kuzifuata.
Sanura alisema TIA Singida ni moja ya kampasi ambayo inapokea wanafunzi kutoka kila mkoa na kueleza kuwa udahili wa wanafunzi umekuwa ukiongezeka kila mwaka.
Alitaja kozi zinazotolewa na chuo hicho kuwa ni Accountancy , Procurement and logistic management, Human resource management, Business Administration na Marketing and public relation.
Aidha, Sanula alisema kozi zote hizo zinaanzia ngazi ya cheti mpaka masters.
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu
chuo hicho unaweza kupiga simu namba 0752540341 au kupitia mtandao wao (Website)
www.tia.ac.tzRais wa Serikali ya Wanafunzi (TAISO) wa chuo hicho, Maiba Loitare,akizungumza.
Mwanasheria wa TIA Singida Wakili Joseph Wawa akizungumza na wanafunzi hao.
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakiwa kwenye tukio hilo.






.jpg)




No comments