TAKUKURU SINGIDA: UFINYU WA NAFASI CHANZO CHA RUSHWA VYUONI
Na Dotto
Mwaibale, Sindida
IMEELEZWA
kuwa ufinyu wa kupata nafasi katika vyuo bora ni moja ya chanzo kinachowafanya
baadhi ya wanafunzi wasio na sifa kutoa rushwa ili kupata nafasi.
Hayo
yamebainishwa na Benjamin Masyaga Afisa
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Singida wakati akitoa Elimu
kuhusu Mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa vyuoni wakati akizungumza na
wanafunzi walioanza msimu wa masomo wa 2025/ 2025 Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA),
Kampasi ya Singida.
“ Ufinyu wa kupata nafasi (udahili) katika vyuo bora baadhi ya wanafunzi wasiokuwa na sifa hutumia mbinu za kihalifu ikiwemo kutoa rushwa kupata nafasi hizo,” alisema Masyaga.
Masyaga
alisema sababu za kuwapo kwa rushwa vyuoni kwa mujibu wa taarifa za utafiti ni
pamoja na ufinyu wa kupata nafasi katika vyuo husika, baadhi ya viongozi wa
vyuo kutochukua hatua zozote dhidi ya walalamikiwa pale wanafunzi wanapotoa
taarifa.
Alitaja
sababu nyingine ni wanafunzi wasiokuwa na ufaulu au sifa za kutosha kutumia
kila mbinu ikiwemo rushwa ili kufaulu mitihani kwa maelezo kuwa shahada hizo
ndiyo mlango wa kupata ajira.
“Sababu nyingine za kuwapo kwa rushwa vyuoni ni kupata majibu ya mtihani kabla ya wakati ambapo wanafunzi wanapewa au wanagundua maswali ya mtihani kabla ya muda wa mtihani kwa malipo ya fedha au zawadi,” alisema Masyaga.
Alisema eneo
lingine la rushwa ni kupata alama za miradi (Tafiti) kw rushwa ambapo wanafunzi
hujaribu kutoa rushwa kwa walimu wa mradi ili kupewa alama nzuri.
Masyaga
alitaja sababu nyingine ya rushwa vyuoni ni baadhi ya wanafunzi kukosa uelewa
wa mapambano dhidi ya rushwa kwa kutohudhuria semina au mafunzo husika.
Akizungumzia kuhusu TAKUKURU alisema ni kifupi cha jina Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11/2007 {PCCA Na. 11/2007}





.jpg)




No comments