Breaking News

NAIBU SPIKA ACHANGISHA MILIONI 5 HARAMBEE YA VYOMBO VYA MUZIKI MANYARA

 

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Daniel Sillo, akizungumza wakati akiongoza harambee ya kuchangia vyombo vya muziki wa injili katika Kanisa Tirano lililopo mkoani Manyara Novemba 23, 2025.

......................................

Na Mwandishi Wetu, Manyara.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Daniel Sillo, Novemba. 23, 2025 ameshiriki harambee ibada katika Kanisa la Tirano lililopo eneo la Galapo Mkoa wa Manyara ambapo alichangisha Sh. Milioni 5.7 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki ambavyo vitatumika kuhubiri injili kwa njia ya uimbaji.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Mhe Sillo alihimiza kudumisha amani iliyopo nchini na kueleza viongozi wa dini ni watu muhimu katika kihubiri amani hiyo kwa waumini wao.

"Kutunza amani ya Taifa letu inawategemea sana viongozi wa dini na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo ikiwa pamoja na kuwaombea viongozi wa nchi,' alisema Sillo.

Mhe. Sillo alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa, kuliombea Bunge, Mahakama, Rais ili nchi yetu iendelee kuwa na amani na kuwawezesha wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wake Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Taifa, Askofu John Margwe akizungumza kwenye harambee hiyo alimshukuru Mhe. Naibu Spika kwa kukubali kuongoza harambee hiyo iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa.

Aidha, Askofu Margwe alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mhe. Sillo kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumtakia kazi njema ya kulitumikia Taifa kupitia nafasi yake hiyo.

Wana kwaya ya Pradise ya kanisa hilo wakittoa burudani ya nyimbo za injili  wakati wa harambee hiyo.
Mchungaji Stephen Kongi akihubiri katika ibada hiyo ambayo iliambatana na zoezi la harambee hiyo.
Furaha na shangwe ikitamalaki kwenye harambee hiyo.
Mhe. Sillo akiwa na muumini wa kanisa hilo.
Mhe. Sillo akisalimiana na waumini wa kanisa hilo.
Viongozi wa kanisa hilo wakimvika mgolole Mhe. Sillo ikiwa ni ishara ya kumpa heshima.
Mhe. Sillo akiwa katika picha ya pamoja na Wana Kwaya ya Paradise ya kanisa hilo.
Mheshimiwa Sillo akipeana mkono na Makamu Askofu wa kanisa hilo, John Margwe.

No comments